Shirika lisilokuwa la Kiserikali la World Vision mkoani Kagera limezindua mradi mkubwa wa maji katika Kata ya Bulembo kijiji cha Bulembo Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

Mradi huo uliogharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 150 umejengwa na Mradi wa Missenyi AP kwa kushirikiana na Jamii ya Kijiji cha Bulenmbo, umezinduliwa na kukabidhiwa kwa Wananchi hao na Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwa katika Ziara yake ya Kikazi Wilayani Missenyi Mkoani Kagera.

Aidha, katika salamu zake akiongea na wananchi, Aweso amewataka kukilinda chanzo hicho na Mradi huo wa maji huku akiwataka watumishi ndani ya wizara hiyo kuiga mfano na kujifunza namna ya usimamizi wa shughuli hizo kwa kubana fedha, lakini kazi yenye matokeo chanya.

Polepole amng'ang'ania Prof. Assad
Simba yaanza kuitafuna JS Saoura ya Algeria taratibu

Comments

comments