Rapa Ambwene ‘AY’ Yesaya, mmoja kati ya wasanii wa Tanzania waliofungua milango ya soko la muziki wa Bongo Flava nje ya nchi ameuelezea urafiki wa damu kati yake na msanii wa Uganda, Jose Chameleon uliopelekea kupeana zawadi kubwa.

Akifunguka katika kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm, AY aliitaja zawadi inayoweza kuwa aghali zaidi kuwahi kutolewa kati ya wasanii wa muziki wa nchi mbili tofauti katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuwekwa wazi.

Alisema Chameleon alimzawadia saa aina ya U-Boat, mwaka jana yenye thamani ya $8000 (zaidi ya shilingi milioni 16 za Tanzania) kutokana na kuguswa na urafiki wao.

“Ile saa ni kama dola 8,000 hivi,” alisema. “Alinipatia akaniambia ‘bwana hii ni saa ambayo nilijinunulia mwenyewe lakini kwa jinsi ambavyo mimi na wewe tumeishi pamoja vizuri miaka mingi, naona ni vizuri kama nikikupatia hii zawadi’. Kwa kweli nilifurahi sana,” alisema AY.

Alisema kuwa wamekuwa marafiki kwa miaka mingi wakiheshimiana na kupeana mawazo na kwamba msanii huyo (Chameleon) alikuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza kuusikia wimbo wa ‘Zigo’ hata kabla haujatoka, na alipanga kushiriki kuifanya Remix yake.

Mbali na Chameleon, wengine waliokunwa na ‘Zigo’ na kutamani kuifanyia Remix ni pamoja na Wizkid.

Rais Magufuli amteua Mrema, atimiza ahadi ya kumpa Kazi
Waziri Mkuu Afungua Duka la MSD Ruangwa, Kuhudumia Hospital 524