Mungu ameendelea kuwa mwema kwa Ambwene ‘AY’ Yesaya na mkewe Remy ambapo jana wamepata mtoto wao wa kwanza.

AY ameiambia dunia kuhusu habari hiyo njema na kueleza kuwa mkewe alijifungua mtoto wa kiume Dallas, Texas nchini Marekani, mtoto waliyempa jina la Aviel, jina ambalo maana yake ni ‘Mungu ni Baba yangu’.

“Mungu ni mwema na namshukuru sana kwa kutubariki mimi na My Beautiful Wife #Remy tarehe 12.08.2018 Medical City Healthcare Dallas -Texas tumepata mtoto wa kiume AVIEL maana yake GOD IS MY FATHER…. 3.9Kgs & 27 inches…Welcome to the World AVIEL YESSAYAH 🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿,” AY ameandika kwenye Instagram.

AY na Remy walifunga ndoa Februari mwaka huu, ndoa iliyotanguliwa na ile ya kimila nchini Rwanda ambako ni nyumbani kwao Remy na kisha ile ya Tanzania iliyohitimisha utaratibu wote wa kuwa wanandoa.

Dar24 tunawapa hongera AY na Remy kwa kupata mtoto. Mungu azidi kuwabariki.

Rais Magufuli afanya teuzi mpya zaidi ya nafasi 41
Picha mpya za Rihanna akiwa ufukweni zamchanganya Chris Brown

Comments

comments