AY Mzee wa Biashara, amewataka wasanii wa Tanzania kufungua macho na kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa mafanikio wanayoyapata hivi sasa sio mafanikio makubwa kama wengi wanavyofikiria.

AY amekiambia kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm kuwa wasanii nchini wanapaswa kujilinganisha na mafanikio ya wasanii wakubwa wa nchi nyingine za Afrika ili kubaini tofauti kubwa iliyopo kati yao.

“Vitu vya kurekebisha vipo vingi, ila inabidi twende mbio mno. Unajua watanzania tumejaliwa kuongea mno kuliko kufanya, so inabidi tufanye. Na ukienda kujichanganya na washikaji wa nchi nyingine ndio unagundua ‘eeh! Kumbe sisi tuko nyuma sana’. Sisi tukiwa wenyewe kwa wenyewe tunajiona tumejimbia but hatujakimbia hivyo,”

AY aliongeza kuwa soko la muziki Tanzania ni kubwa kuliko masoko ya nchi nyingine za Afrika Mashariki, hivyo wasanii wana nafasi zadi ya kufanya biashara endapo watafanya kazi na kuangalia mbali zaidi ya mtazamo uliopo hivi sasa.

Alisema kuwa binafsi aliwahi kupiga hatua kubwa ambayo kama wasanii wa Tanzania hawatafunguka na kuanza kukimbia zaidi, hawataweza kuifikia kamwe.

“Kwanza shout out to ma Ninja Fid Q, mwaka 2009 nilikuwa katika tuzo za MTV, Category yangu ilikuwa mimi, Jay Z, Kanye West, M.I na Zulu Boy. Kwa hiyo nikamwambia Fid ‘haitawahi kutokea tena hii’,” alisema AY.

Ambwene ambaye hivi sasa wimbo wake wa ‘Zigo’ umekuwa gumzo katika nchi nyingi za Afrika huku akiombwa na wasanii wakubwa kuifanyia Remix, amesema wasanii wa Tanzania wanapaswa kuongeza bidii na kuhakikisha ‘identity’ ya muziki wa Tanzania haipotei ili kupata soko la kudumu duniani.

 

 

 

 

 

 

 

Stoke City Wakamilisha Usajili Wa Shaqiri
Daktari Eva Carneiro Apigwa Stop Chelsea