Klabu ya Azam FC imethibitisha taarifa za Mshambuliaji Ayoub Lyanga kuingia katika chumba cha upasuaji leo Jumanne (Novemba 16) asubihi katika Hospitali ya Life Vincent Pelloti mjini Cape Town- Afrika Kusini.

Azam FC imethibitisha taarifa za mshambuliaji huyo kuanza matibabu kwa kuweka taarifa kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii na kuandika: #KilaLaHeri Winga wetu, @lyanga23 muda huu ameingia chumba cha upasuaji huko Afrika Kusini katika hospitali ya Life Vincent Pelloti mjini Cape Town.

Upasuaji wake unatarajiwa kuchukua saa mbili.

Lyanga aliumia Novemba pili mwaka huu kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold.

Simba SC yashauriwa kusajili dirisha dogo
Breaking News: Soko la Manzese Tunduma laungua