Asasi za Kiraia zinazotekeleza Miradi ya afya katika Mkoa wa Mwanza na Shinyanga zimetakiwa kuendeleza desturi ya kufanya kazi kwa kushirikiana na Halmashauri, ili kushirikisha jamii katika uimarishaji wa huduma bora za afya na kuleta mabadiliko chanya.

Wito huo, imetolewa leo Januari 30,2023 Wilayani Sengerema mkoani Mwanza  na Mratibu wa Huduma za Afya katika jamii kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Martha Mariki katika ufunguzi wa mafunzo ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii (Community Score Card).

Amesema, “ni muhimu Asasi za Kiraia kushirikiana  na Serikali  katika kuwezesha Maendeleo hususan  Sekta ya Afya usipoweza kufanya community Empowerment wananchi watakuwa tegemezi badala ya wao kushiriki kufanya mambo fulani ya kuleta maendeleo na watakuwa wanaisubiri serikali kupeleka huduma.”

Aidha, Martha ameongeza kuwa ni muhimu kufanya kazi kama timu baina ya serikali na asasi mbalimbali za kiraia, ili kuleta ufanisi katika sekta ya Afya.

Polisi yawaonya wafugaji kuhamisha mifugo bila utaratibu
Wadau watakiwa kuweka mkakati ulinzi kwa Watoto