Azam FC itacheza mechi ya kirafiki Jumamosi ijayo kujiandaa na mchezo wa robo fainali ya FA dhidi ya Mtibwa Sugar utakayofanyika uwanja wa Azam Complex mwisho wa mwezi huu.

Azam iliingia kambini wiki iliyopita kujiandaa na mchezo huo kipindi hiki ligi ikiwa imesimama kupisha mechi za kirafiki za kimataifa zilizo kwenye kalenda ya FIFA.

Ofisa habari wa Azam FC, Jaffer Idd amesema kuwa timu inaendelea kujifua kujiwinda na mchezo huo ambao wanatarajia utakuwa mgumu kutokana na uimara wa wapinzani wao.

Jaffe amesema timu watakayo cheza nayo wataitangaza siku chache zijazo huku mechi hiyo ikitarajiwa kupigwa katika uwanja wa Azam Complex.

“Tunatarajia kuwa na mchezo wa kirafiki siku ya Jumamosi ili mwalimu aone wachezaji wake wanaelewa vipi mafunzo anayo wafundisha.

“Kufanya mazoezi peke yake haitoshi bila kupata mechi za kujipima nguvu, kwa sasa nguvu zetu tunaelekeza FA na mechi itakuwa dhidi ya Mtibwa,” alisema Jaffer.

Hotuba ya Rais wa TFF alipozungumza na wahariri wa habari za michezo
Kikwete: Viongozi Simba SC, Young Africans mjitathmini