Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam FC itakutana uso kwa uso na vigogo wa soka Esperance Sportive de Tunis kutoka nchini Tunisia, katika mchezo wa raundi ya pili ya mtoano kwenye kombe la Shirikisho Barani Afrika ‘CAF Confederations Cup’.

Azam ilifanikiwa kukata tiketi ya raundi hiyo baada ya kuibomoa klabu ya Bidvest Wits maarufu kama ‘The Clever Boys’ kutoka Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 7-3.

Esperance wao walifanikiwa kutua raundi hiyo baada ya kuitoa Renaissance FC kutoka nchini Chad kwa kipigo kikali cha mabao 7-0.

Pambano hili kali kati ya Azam na Esperance linarajiwa kuchezwa kati ya tarehe 8-10 Aprili huku mchezo wa kwanza ukichezwa jijini Dar es salaam, na mshindi wa raundi hiyo ya pili ya mtoano atafanikiwa kukata tiketi ya kuingia hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Barani Afrika mwaka huu.

Haruna Niyonzima Kuwakosa Waarabu Wa Misri
Jahazi La Man City Linavyoendelea Kuzamishwa Na Majeruhi