Uongozi wa Azam FC umekanusha taarifa za kuwa mbioni kusitisha makataba wa Kocha wao kutoka nchini Zambia George Lwandamina.

Mara baada ya mchezo wa mzunguuko wanne wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Young Africans uliochezwa Jumamosi (Oktoba 30) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Lwandamina alihusishwa na taarifa za kuwa kwenye nafasi mbaya klabuni hapo.

Leo Jumanne (Novemba 02), Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amekanusha taarifa hizo, na kusema sio za kweli.

Hata Hivyo Zaka Zakazi amethibitisha taarifa za mkataba wa kocha Lwandamina kufikia kikomo, lakini amesisitiza Uongozi wa Azam FC upo katika mpango wa kumsainisha mkataba mpya.

“Kiukweli sina taarifa kama kocha anataka kufukuzwa ndiyo maana hizo ni tetesi ila hakuna hata mpango wakuondolewa.”

“Mkataba wake umeisha na atasaini mkataba mwingine wa mwaka mmoja wa kuendelea kusalia Azam,” amesema Zaka Zakazi.

Azam FC imekua na mwenendo mbaya tangu ulipoanza msimu huu 2021/22, baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union, kupoteza dhidi ya Polisi Tanzania mabao 2-1, kushinda dhidi ya Namungo FC 1-0 kabla ya kupoteza dhidi ya Young Africans kwa mabao 2-0.

Upande wa Michuano ya Kimataifda (Kombe la Shirikisho) Azam FC waliondoshwa na Pyramids FC ya Misri kwa kufungwa 1-0, baada ya kuitoa Horseed FC ya Somalia kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1.

TFF yakemea vurugu viwanjani
Video: Dakika 3 za Rais Samia COP 26