Uongozi wa Azam FC umekanusha taarifa za kuwa kwenye mpango wa kumtimua Kocha George Lwandamina na nafasi yake kuchukuliwa na aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Patrick Aussems.

Jana Alhamis (Novemba 25) taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zilieleza kuwa, Azam FC wapo mbioni kumuajiri Patrick Aussems ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha AFC Leopard ya nchini Kenya.

Mapama leo Ijumaa (Novembe 26), Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Azam FC Thabit Zacharia ‘ZakaZakazi’ amekanusha taarifa hizo alipohojiwa na Wasafi FM kupitia kipindi cha Michezo Sports Arena.

Zaka amesema taarifa za Azam FC kuwa kwenye mchakato wa kumsaka mbadala wa Lwandamina sio za kweli, kwani wataendeelea kufanya kazi kocha huyo kutoka Zambia.

Kuhusu tetesi za Aussems kuajiriwa klabuni hapo, Zaka amesema Kocha huyo aliwahi kuomba kazi katika klabu hiyo lakini hakupewa kibarua hicho, na hawana mpango wa kumrejesha nchini kufanya kazi huko Azam Complex Chamazi.

Amesema hawamuhitaji Aussems kwani matokeo yao mabaya uwanjani yanatokana na maandalizi hafifu katika kipindi Cha mapumziko na shida sio kocha.

Mbeya Kwanza FC yaandaa ZAWADI NONO
WHO kujadili kirusi kipya cha corona