Azam FC imeamua kuachana na kipa wake mkongwe Ivo Mapunda waliyemsajili msimu uliopita kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake, huku wakifanya mchakato wa kumsajili kipa mwingine.

Ivo ambaye ni kipa mkongwe alitua Azam FC msimu uliopita akitokea Simba baada ya kushindwa kumsajili katika dakika za mwisho ambapo wanalambalamba hao waliamua kumpa mkataba wa mwaka mmoja.

Katibu Mkuu wa Azam FC, Idrisa Nassor amesema kuwa, hawataendelea na Ivo msimu ujao wa ligi kuu na kwa sasa wanafanya mchakato wa kusajili kipa mwingine atakayeziba nafasi yake.

“Hatutarajii kuendelea na Ivo msimu ujao wa ligi kuu na badala yake nafasi yake itachukuliwa na kipa mwingine ambaye tunafanya mchakato wa kumsajili ili kuziba nafasi hiyo.

“Kwa sasa amebakiza miezi mitatu ili kukamilisha mkataba wake na Azam aliosaini mwaka mmoja msimu uliopita na baada ya hapo tutaangana alisema bosi huyo.

Chanzo: Championi

Waziri Mpango Awataka (TCRA,TRA na BOT) Kushirikiana.
Gwajima kuendelea Kusakwa Popote Alipo''