KIKOSI cha Azam FC kimewasili jijini Tanga tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Maafande wa JKT Ruvu utakaofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kesho Jumamosi.

Azam chini ya kocha Aristica Cioba ilisafiri na nyota 20 na kuwasili mjini Tanga usiku wa kuamkia leo, ambapo wamefikia kwenye hoteli ya Mtendere ili kuwavutia kasi Maafande hao.

Wachezaji hao ni walinda mlango Aishi Manula na Metacha Mnata walinzi ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Daniel Amoah, Ismail Gumbo, Gadiel Michael, Bruce Kangwa na Abdallah Kheri.

Viungo ni Himid Mao, Abubakar Salum, Frank Domayo, Masoud Abdallah, Mudathir Yahaya, Joseph Mahundi, Ramadhan Singano na Hamis Mcha huku washambuliaji wakiwa Shaban Idd na Samwel Afful.

Azam watashuka kwenye mchezo huo wakiwa nafasi ya tatu baada ya timu ya Kagera Sugar kupokonywa pointi tatu kutokana na kumchezesha beki Mohammed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za njano.

Mzunguko wa kwanza wa ligi na baadhi ya michezo ya duru ya pili, Ruvu JKT walikuwa wakitumia uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani lakini baada ya nusu ya wachezaji wake ambao ni waajiriwa wa jeshi kuhamishiwa mkoani Tanga wakaiomba TFF kutumia uwanja wa Mkwakwani kama dimba la nyumbani.

Mourinho Awachana Washambuliaji Man Utd
Mbwana Samatta Ashindwa Kufurukuta Hispania