Klabu ya Azam FC imewaongezea mkataba makocha wake watatu wanaounda benchi la ufundi, kwa ajili ya kuendelea kuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2020/21.

Kocha Mkuu Aristica Cioaba kutoka Romania  amekamilisha mpango huo sanjari na wasaidizi wake Bahati Vivier wa Burundi na Kocha wa Viungo, Costel Birsan.

Taarifa kutoka Azam FC zimeeleza kuwa, makocha hao wamesaini mkataba wa mwaka mmoja kila mmoja.

Mwishoni mwa juma lililopita Azam FC waliwatambulisha wachezaji wao wapya pamoja na benchi la ufundi ambalo lilianza kazi kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Namung FC, Uwanja wa Azam Complex.

Kwenye mchezo huo uliohudhiuriwa na mashabiki wengi, Azam FC ilishinda mabao mawili kwa moja, na kuipa upinzani mkali Namungo FC ambayo itacheza mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii mwishoni mwa juma hili dhidi ya Simba SC, mjini Arusha.

Kocha msaidizi Bahati Vivier.

Kocha wa Viungo, Costel Birsan
Safari ya JPM kugombea Urais
Sven: Kutakuwa na ushindani mkubwa Simba SC