Uongozi wa Azam FC unaamini wimbi la majeruhi lililowakumba msimu huu, ni sehemu ya sababu zilizokifanya kikosi chao kushindwa kufikia lengo la kuwa katika nafasi nzuri za kupambania ubingwa.

Azam FC ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na alama 32, zilizotokana na ushindi mara 09, kufungwa mara 09 na kutoka sare mara 05.

Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo yenye maskani yake makuu Chamazi jijini Dar es salaam Jonas Tiboroha amesema kuwa, majeruhi ya wachezaji ndio kumeathiri matokeo ya klabu mpaka sasa.

Amesema changamoto hiyo imekua ikijirudia mara kwa mara katika kipindi cha msimu huu, ambapo baadhi ya wachezaji wao muhimu walilazimika kuwa nje kwa zaidi ya majuma matatu hadi manne.

“Tatizo kubwa ambalo tumeliona hapa Azam FC ni majeruhi, wachezajai wengi walipatwa na majeraha ya muda refu na kuiacha timu ikiwa katika wakati mgumu, tunajifunza kutokana na changamoto tunazozipitia kwa sasa.”

“Suala la majeraha sio la kupanga, bali huwa linatokea kutokana na uhalisia wa mchezo wa soka, lakini tutajitahidi kuwa na mpango ambao utatuwezesha kuwa na wachezaji wenye kulingana viwango kuanzia msimu ujao.”

“Lengo letu ni kufanya vizuri kama vilabu vinavyokimbizana kwenye ubingwa, lakini msimu huu imekua bahati mbaya sana kwa Azam FC, ila tunajiapanga kwa kushirikiana na idara zote ndani ya klabu ili kufikia malengo yetu kuanzia msimu ujao.” amesema Tiboroha

Azam FC inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzani Bara Mzunguuko wa 24 dhidi ya Mabingwa watetezi Simba SC utakaopigwa katikati ya juma lijalo Uwanja wa Azam Complex.

Bernard Morrison bado anaitaka Simba SC
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 13, 2022