Michuano ya Kombe la Mapinduzi ilichoanza kutimua vumbi jana jioni kwenye dimba la Amani, Zanzibar, imeendele tena leo jioni, lakini wengi wanaitolea macho zaidi mechi ya kesho Jumanne.

Hiyo ni kwakuwa, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam wataonyeshana kazi na Azam FC ambayo imejitokeza kuwa na upinzani wa haja kwa Yanga.

Mchezo wa miamba hiyo inayotokea katika jiji la Dar es Salaam, unavuta hisia za wengi kutokana na ushindani uliopo baina ya vikosi vya timu hizo kwa sasa.

Wadau wengi wa soka walisema, wangetamani kuziona timu hizo zikikwaana katika mechi ya fainali, lakini kwa kuwa ratiba imelazimisha watamiminika uwanjani kuzishuhudia.

Mashabiki wa soka visiwani Zanzibar watamiminika kwa wingi uwanjani wakiwa na shauku kubwa ya kushuhudia mtanange kati ya timu hizo utakaopigwa saa 2:30 usiku.

Zilipokutana katika mechi tatu za hivi karibuni zilitoshana nguvu kwa kutoka sare mara zote, wakianzia Kombe la Kagame ambapo Azam ilibidi watwae ubingwa kwa penati na kwenye Ngao ya Jamii zilitoka sare na Yanga kubeba kwa penati kabla ya kutoka 2-2 kwenye mzunguuko wa kwanza wa Ligi Kuu.

Matokeo hayo ndio yanayoongeza kiu ya mashabiki katika kujua mbabe baina ya timu hizo ni yupi, ambapo ni suala la kusubiri kuona.

Vinara Wa Ligi Ya La Liga Wafikiria Kumrejesha Shujaa Wao
Mugabe, Museven Watahadharishwa kufungwa jela na Mgombea Urais Wa Marekani