Azam FC imeng’olewa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kutandikwa mabao 2-1 dhidi ya Mafunzo katika mechi ya mwisho ya makundi.
Azam FC ilikuwa ya kwanza kufunga kupitia kwa Kire Tchetche, lakini ikakubali mabao mawili katika kipindi cha pili na kung’olewa katika michuano hiyo.
Katika mechi za makundi kutoka Kundi A, Azam FC imetoka sare mechi mbili dhidi ya Mtibwa Sugar na Yanga, halafu ikatwangwa na Mafunzo hivyo kuwa na pointi mbili tu.
Yanga na Mtibwa Sugar ambazo zinakutana usiku, zote kila moja ina pointi nne hivyo zimejihakikishia kufuzu nusu fainali.
Azam FC sasa ndiyo inashika mkia ikiwa na pointi mbili, huku Mafunzo ikiwa na pointi tatu.

 

Kaijage Wa Twiga Stars Atangaza Kujiweka Pembeni
Wajifungia Kuisuka Upya Chadema