Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Farid Mussa Malik amefaulu majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania.

Mkurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa anayefuatilia majaribio ya mchezaji huyo Hispania, na kuthibitisha kwamba CD Tenerife sasa inatarajiwa kuingia katika mazungumzo na klabu yake juu ya kumnunua mchezaji huyo.

“Tunatarajia kuanza mazungumzo nao juu ya suala la Farid, ingawa wazo lao la awali ni kumchukua kwa mkopo wa miaka miwili. Sasa tunasubiri ofa yao rasmi, kisha Bodi ya Ukurugenzi itajadili na kutoa maamuzi,”amesema Bakhresa.

Kwa upande wake, Farid amefurahia matokeo hayo na kusema haikuwa kazi nyepesi kwake kuweza kuwaridhisha maofisa wa benchi la ufundi la Tenerife.

“Kwa kweli nimefurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa kufuzu majaribio, ila haikuwa kazi nyepesi, mpira wa Ulaya mgumu,”amesema.

Awali, Farid ilikuwa apelekwe moja ya klabu za Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga, kati ya Las Palmas na Athletic ya Bilbao kwa majaribio, lakini wakala wake akashauri mchezaji huyo aanzie timu ya Daraja la Kwanza Hispania ili kupata nafasi ya kucheza na kuinuka haraka.

Aitor Karanka Atibua Mazingira ya Kazi Yake Riverside Stadium
Lissu achafua hali ya hewa Bungeni, aivaa serikali na 'Hapa Kazi Tu'