Uongozi wa klabu ya Azam FC umetoa ufafanuzi wa kutoa basi lao kwa timu ya Al Masry kuwa ni kutokana na kupokea barua kutoka kwa Simba kulihitaji kwa ajili ya Waarabu hao toka Misri.

Basi hilo lilionekana uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere likiwabeba wachezaji wa Al Masry asubuhi ya leo baada ya kutua nchini kitu kilichodhaniwa huenda Azam wanaisaidia Masry kuia Simba.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema kuwa, uongozi kupitia kwa Mkurugenzi wao Mtendaji ulipokea barua kutoka Simba ikiwaomba kuwapa basi wapinzani wao kwa ajili ya usafiri kwa muda wote watakaokuwa nchini.

“Hatuna undugu wala urafiki na Al Masry kilichotokea ni Simba wenyewe walituomba basi na kwakua kipindi hiki timu ipo mjini tumekubali kuwapa,” alisema Jaffer.

Jaffer alisema sio mara ya kwanza kwa basi hilo kutumiwa na timu kutoka nje kwani mara kadhaa wamekuwa wakifanya hivyo kwa timu za Taifa zinakuja kucheza na Stars.

Mrema adai Tahliso wanatumika
Mkwasa: Tunaitakia kila kheri Simba dhidi ya Al Masry