Azam FC imeendelea kujizatiti kimaandalizi kuelekea mchezo wake dhidi ya Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC, utakaocheza Julai 14 Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Azam FC leo Jumamosi (Julai 10) imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Trans Camp inayoshiriki Ligi Daraja La Kwanza.

Mchezo huo ambao ni maandalizi ya kuelekea pambano dhidi ya Simba SC, umechezwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi na kushuhudia wenyeji Azam FC wakichomoza na ushindi wa mabao 2-1.

Huu ni mchezo wa pili wa kirafiki kwa Azam FC, ukitanguliwa na ule dhidi ya Pamba FC kutoka jijini Mwanza.

Azam FC imebakisha michezo miwili ya Ligi Kuu msimu huu 2020/21, dhidi ya Simba SC na Ruvu Shooting.

Maandamano ya kumtoa Zuma jela yafikia pabaya
Matola: Mchezo utakuwa mgumu