Ombi la uongozi wa klabu ya Young Africans la kutaka kumtumia mshambuliaji Adam Salamba katika michuano ya kombe la shirikisho hatua ya makundi, huenda likawekwa kapuni na Lipuli FC, kufuatia Azam FC kuingilia kati mpango huo kwa kutuma ofa ya usajili wa mshambuliaji huyo.

Azam FC wamethibitisha mpango huo hii leo kupitia idara ya habari na mawasilino inayoongozwa na Jaffar Iddy Maganga, ambapo amesema, tayari wameshawasilisha ofa yao mjini Iringa yalipo makao makuu ya klabu ya Lipuli FC, ambayo msimu huu imeshiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza, baada ya miaka kadhaa kupita.

Jaffer amesema kuwa bechi la Ufundi la klabu ya Azam FC limevutiwa na ubora wa mshambuliaji huyo, na wanaamini atakuwa msaada mkubwa kwenye kikosi chao msimu ujao kama watafanikiwa kumpata.

“Sisi kaka Azam FC tumemfuatilia kwa karibu Adam Salamba na tumeona ana uwezo wa kuichezea timu yetu kwa msimu ujao wa ligi,” amesema Jaffar

“Tumeshawaandikia barua Lipuli FC ili kuangalia namna ya kuanza mazungumzo ya kumsajili mchezaji huyo, maana tunafahamu utaratibu na kanuni za mchezo wa soka pindi unapohitaji huduma ya mchezaji anaemilikiwa na klabu nyingine.

Young Africans iliandika barua kwenda Lipuli FC kutaka kumuazima Adam Salamba ili wamtumie kwenye mchuano ya kombe la shirikisho ila klabu ya Lipuli imekaa kimyaa kujibu barua hiyo ikihofia iwapo Salamba ataenda kucheza Young Africans anaweza akagoma kurudi.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 16, 2018
Rais Magufuli kukabidhi kombe la Ubingwa 2017/18