Sare ya bila kufungana (0-0) dhidi ya Mwadui FC, imeaitisha hafakati za klabu ya Azam FC kuwa mabingwa msimu huu 2020-21.

Azam FC wakiwa ugenini mjini Ruangwa mkoani Lindi jana Jumatatu (Julai 21), walilazimishwa sare hiyo na kujikuta wakifikisha alama 64 nyuma ya Young Africans yenye alama 67, ikitangtuliwa na Simba SC yenye alama 70.

Azam FC imesaliwa na michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu huu, na endapo itafanikiwa kushinda michezo hiyo, itafikisha alama 70, ambazo kwa sasa zinamilikiwa na Simba SCinayoongoza msimamo wa Ligi hiyo.

Simba SC bado ina michezo sita na inahitaji alama moja kuikimbia Azam FC kwenye mbio za ubingwa, huku ikitarajiwa kucheza dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam, leo Jumanne (Juni 22).

Ni dhahir mbio za ubingwa zimesalia kwa Simba SC na Young Africans yenye alama 67, huku ikibakisha michezo mitatu mkononi.

Katika hatua nyingine Simba SC inahitaji alama moja tu kujihakikishia nafasi ya Kushiriki Michuano ya klabu bingwa barani Africa.

Uhakika wa Simba SC kuhitaji alama moja umetokana na.matokeo ya Azam FC dhidi ya Namungo FC.

Tanzania itawakilishwa na timu mbili kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika, na timu mbili kwenye michuano Komba la Shirikisho.

Man City yatupa ndoano
Ajali ya gari yaua Saba Morogoro