Hatimaye Uongozi wa Azam FC umethibitisha kuachana na baadhi ya wachezaji wake wa Kimataifa, kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021-22.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hiyo, wachezaji walioachwa ni beki wa kati, Yakubu Mohammed, kiungo Ally Niyonzima, mshambuliaji Mpiana Monzinzi na Obrey Chirwa, ambaye mkataba wake umemalizika.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa: Tumefikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na wachezaji wetu wanne wa kimataifa.

Azam FC tunawashukuru kwa mchango wao waliotoa katika klabu hii bora kipindi chote walichokuwa nasi na tunawatakia kila la kheri huko waendako.

Dkt Mpango ashiriki misa ya kumbukizi ya Hayati Mkapa
Mradi chujio la maji kukamilika September 2021