Inaelezwa kuwa Uongozi wa Azam FC umedhamiria kumsajili Kiungo wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Feisal Salum ‘Fei toto’ mwishoni mwa msimu huu.

‘Fei toto’ amekua akitajwa kuwa kwenye mipango ya Klabu hiyo ya Chamazi jijini Dar es salaam, huku tajiri Yusuph Bakhresa akitajwa kuwa mstari wa mbele, kuhakikisha anamsajili kiungo huyo kwa gharama yoyote.

Mtu wa karibu na Uongozi wa Azam FC amefichgua siri hiyo kwa kusema tayari viongozi wamejipanga kuipata saini ya ‘Fei toto’ na kama mambo yatakwenda kama yalivyopangwa watafanikiwa kwa asilimia 100.

“Azam FC iko tayari kutoa ofa kubwa ambayo itakuwa na thamani mara tatu au tano ya kiasi cha fedha anacholipwa sasa mchezaji huyo na klabu ya Young Africans,”

“Matajiri wamefika mbali wameshafanya mazungumzo na familia yake (Mama mzazi wa Fei Toto) na mama ameridhia mwanae kuhamia Azam FC.” ameeleza mtu huyo ambaye hakuwa tayari jina lake kutajwa katika vyombo vya habari.

Hata hivyo Uongozi wa Young Africans haujasema lolote hadi sasa kuhusu mpango wa kukubali ama kukataa kumuuza ‘Fei toto’, na badala yake umeendelea na mkakati wa kuhakikisha wanatetea ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu 2022/23.

Juma Mgunda: Sitafanya mzaha Kombe la Shirikisho
Edna Lema arudisha ujumbe Young Africans