Kikosi cha Azam FC kimewasili salama mjini Bukoba mkoani Kagera tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaoshuhudia wakiparangana dhidi ya Kagera Sugar.

Mchezo huo unaotarajiwa kuwa na vuta ni kuvute utachezwa kesho Jumatano (Machi 03) Uwanja wa Kaitaba, huku Azam FC wakiwa na lengo la kuhakikisha wanapata ushindi ugenini, ili hali wenyeji wao watakuwa na mikakati ya kubakisha alama tatu nyumbani.

Kikosi cha wachezaji 30 cha Azam FC kiliondoka jijini Dar es salaam leo asubuhi kwa usafiri wa ndege, na leo jioni kinatarajiwa kufanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Kaitaba, chini ya kocha George Lwandamina.

Wachezaji wa Azam FC waliosafiri hadi mjini Bukoba ni Obrey Chirwa, Prince Dube, Hamoudoun, Kangwa Bruce, Braison Raphael, Omary, Wadada, Mudhathir, Nado, Awesu, Daniel, Abdalah na  Lyanga.

Wengine ni Maseke, Niyonzima, Tigere, Aziz, Charlse Emmanuel, Emmanuel Kabelege, Mathias Kigonya, George Lwandamina, Mohamed Yakub, Moris Agrey, Mpiana Monzinzi, Abubakar Idd, Vivier Bahati, Charandura Nyasha, Luckson Jonathan, Vincent Madenge na Nzawila Yusuph

Azam FC ilishinda mchezo wake uliopita wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Mbuni FC waliokubali kufungwa 1-0, na kutinga hatua ya 16 Bora ya Michuano hiyo, huku Kagera Sugar wakiifunga Eagle SC 2-0.

Azam FC inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha alama 37 baada ya kushuka dimbani mara 21, na Kagera Sugar wako nafasi ya 11 kwa kumiliki alama 24 zilizotokana na michezo 21 waliocheza.

TCRA kudhibiti utoaji huduma za vifurushi
Simba SC: Manula yupo salama