Uongozi wa Azam FC umekanusha taarifa za kufanya mazungumzo na mchezaji wa FC Platinum Perfect Chwikwende na mlinda mlango wa Biashara United Mara, Daniel Mgore.


Wawaili hao wanatajwa kuwa kwenye rada za Azam FC katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili, ambapo Azam FC tayari wameshatangaza kuwa wataongeza wachezaji wengine wawili, baada ya kumsajili mshambuliaji kutoka DR Congo Mpiana Monzinzi.


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Zakaria Thabit amesema taarifa za uongozi wa klabu hiyo kufanya mazungumzi na wachezaji hao zinapaswa kupuuzwa, japo wana mpango wa kuendelea kukitumia kipindi hiki kwa ajili ya kukiongozea nguvu kikosi chao.


“Kuhusu Chikwende na Magore bado hatujazungumza nao, hizi taarifa zinapaswa kupuuzwa katika kipindi hiki ambacho fununu huwa nyingi sana kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari.”


“Tutafanya usajili mzuri kwani sifa ya timu kubwa ni kusajili, wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.” Amesema Thabit.


Chikwende ambaye aliifungia FC Platinum bao la ushindi dhidi ya Simba SC kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya mabingwa barani Afrika mjini Harare, Zimbabwe majuma mawili yaliyopita, kwa sasa yupo Tanzania kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili, utakaochezwa keshokutwa Jumatano (Januari 06).


Magore ambaye amekua muhimili mkubwa kwenye lango la Biashara United Mara msimu huu 2020/21, jana alikua dimbani wakati timu yake ilipoibanjua Gwambina FC bao moja kwa sifuri, mjini Misumngwi, mkoani Mwanza.

Maguri: Tumekuja kupambana
Naibu waziri aagiza meneja RUWASA kusimamishwa kazi