Klabu ya soka ya Azam FC imewashusha mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga kwenye msimamo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC kwenye mchezo wa jana usiku.

Katika mchezo huo wa raundi ya 22 kwa Azam FC uliopigwa kwenye dimba la Chamanzi, bao la kwanza lilifungwa na Idd Kipagwile dakika ya 63, kabla ya mshambuliaji Bernard Arthur, kufunga bao la pili dakika ya 72.

Bao pekee la Mbao FC lilifungwa na mchezaji, James Msuva, ambaye ni mdogo wake na nyota wa timu ya Difaa El Jadida Simon Msuva, dakika ya 89.

Adha, Ushindi huo ambao ni wa tatu mfululizo kwa Azam FC ikiwa nyumbani, unaifanya timu hiyo sasa kufikisha alama 44 na kupaa hadi nafasi ya pili, ikiwaondoa Yanga wenye alama 43 huku Simba ikiwa kileleni na alama 46.

Hata hivyo, Baada ya mchezo huo timu ya Azam FC itaanza maandalizi ya mchezo wa robo fainali ya kombe la shirikisho (ASFC) dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Machi 30 mwaka huu kwenye dimba la Chamazi.

Hongera Chege kwa kupata kabinti
Urusi yafanya jaribio la Kombola lisilozuilika

Comments

comments