Azam FC imeamua kuwatimua makocha wake wa kigeni wakiongozwa na kocha mkuu Zeben Hernandez kutoka Hispania.

Uamuzi wa Azam umekuja baada ya mfululizo wa matokeo mabovu kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu huu tangu ‘wahispaniola’  hao  walipokabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo baada ya Stewart Hall kubwaga manyanga.

“Uongozi wa Azam FC umewatimua makocha wao leo mchana baada ya pande zote mbili kukubaliana kuvunja mkataba kutokana na matokeo mabaya kwenye ligi tangu walipowasili.

Katika mechi 17 za VPL ambazo Hernandez alisimama kama kocha mkuu wa Azam FC, timu hiyo imeshinda mechi saba (7), imetoka sare mara sita (6) na kupoteza michezo minne (4).

Zahor: Asante 'President', Ila….
Video: Zantel yatii agizo la Hapi, yalipa deni lililodumu miaka 7