Kipindi cha luninga cha Yanga TV Show kitaanza kuonekana Azam TV kuanzia Aprili Mosi mwaka huu.

Kipindi hicho kitaandaliwa na Yanga wenyewe na kutangazwa na watangazaji kutoka Yanga huku Azam TV ikirusha tu.

Mkurugenzi wa vipindi vya michezo wa Azam TV, Baruhan Mhuza amesema wameingia mkataba wa miaka mitatu na mabingwa hao kurusha shoo hiyo huku alishindwa kuweka wazi gharama yake.

Baruhan amesema kipindi hicho kitakuwa cha dakika 30 na muonekano bora huku akiiusifu uongozi wa Yanga kwa kuandaa studio safi ya TV kwa ajili ya show makao makuu ya klabu.

“Tumeingia mkataba na Yanga kuonyesha Yanga TV Show kuanzia Aprili mosi na itarushwa kupitia Azam Sports Two muda kipindi bado haujapangwa,” alisema Baruhan.

Yanga inakuwa timu ya tatu inayoshiriki ligi kuu kuwa na kipindi cha TV kinachorushwa na Azam TV baada ya Simba na Azam.

Pierre Lechantre kufumua kikosi mwishoni mwa msimu
Dismas Ten awatolea uvivu mashabiki wa Yanga