Awamu ya pili ya wachezaji watano wa Azam FC waliokuwa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, imewasili nchini Zimbabwe kwa ajili ya maandalizi ya kukabiliana na Triangle United.

Hivyo basi kikosi cha Azam FC kipo kamili  baada ya msafara ya kwanza kuongozwa na mkufunzi msaidizi wa timu hiyo Idd Cheche kutangulia kwaajili ya  kuweka mambo sawa.

Wachezaji hao wameungana na wenzao ambao walitangulia awali kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho utakaopigwa Septemba 28.

Wachezaji hao walibaki nchini ni wale waliotumikia timu ya taifa iliyocheza na Sudan uwanja wa Taifa mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Chan.

Wachezaji hao ni Frank Domayo ‘Chumvi’, Mudathir Yahya na Shaaban Chilunda, ambao wameanza mazoezi huku kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije, akiwapumzisha kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na winga Idd Seleman ‘Nado’.

IGP Sirro awaagiza ma-RPC, OCD kutembelea na kutatua changamoto za wananchi
Serikali inapika mpango wa kuboresha mitaala ya elimu nchini