Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC inatarajia kukipiga dhidi ya Mabatini Kombaini katika mchezo wa kirafiki unaotarajia kufanyika leo katika uwanja wa Alliance saa 10.00 jioni.

Kikosi cha Azam FC kipo mkoani Mwanza kikifanya maandalizi ya kuikabili Mbao, katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) unaotarajia kufanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na kombe la Mapinduzi msimu uliopita wanatarajia kuutumia mchezo huo wa kirafiki kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wao na Mbao.

Wachezaji wote wa Azam FC wako fiti, isipokuwa kipa Razak Abalora, anayesumbuliwa na Malaria lakini hapo jana alianza mazoezi mapesi wakati kikosi hicho kilipofanya mazoezi katika uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza.

Azam FC ipo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa ni miongoni mwa timu nne zilizokaa kileleni zote zikiwa na pointi 12, zingine zilizojuu yake zikiwa ni Simba, Yanga na Mtibwa Sugar, ambazo ziko juu yake kwa idadi ya mabao ya kufunga.

Ngemela akiri CCM kuyumba uchaguzi mkuu 2015
Babu Seya amuomba JPM kupitia faili lake