Baada ya kuwa nje ya mchezo wa tenesi kwa muda wa mwaka mmoja Victoria Azarenka anatarajia kurejea uwanjani leo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alipumzika ili kuweza kumlea mwanae baada ya kujifungua na mara ya mwisho kucheza ilikuwa ni katika michuano ya Ufaransa mwaka 2016.

Akiongea na vyombo vya habari Azarenka amesema ”Bado sijapoteza morali wa kupambana na huu ni mwanzo wangu mpya wa kuendeleza kipaji changu”

Azarenka atachuana na Mjapani Risa Ozaki katika raundi ya kwanza ya michuano ya wazi ya Malloca.

Katy Perry afikisha wafuasi milioni 100 twitter
Julio afyatuka tena, amtaka Malinzi aachie ngazi TFF

Comments

comments