Mwanaume mmoja raia wa Zambia aliyetambulika kwa jina la Martin Stampa, anadaiwa kuanguka na kuzirai baada ya kugundua kuwa mke wake ndiye “mwenye nyumba” wake.

Kulingana na taarifa za mitandao ya kijamii nchini humo, imesema, Stampa (37), aliishi katika nyumba hiyo kwa miaka 15, na alikuwa akilipa kwacha 3500 kila mwezi ambazo mkewe alidai kuzipeleka kwa mwenye nyumba wao.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa ugomvi ulizuka baada ya bibi huyo aliyetambulika kwa jina la Lombo Lushomo (27), kugundua kuwa mumewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa.

Mitandao hiyo, inaarifu kuwa Martin Stampa alimwambia mke wake kuwa alipata kimada kwa sababu alitaka mtu mwenye akili na anayejihusisha na mazungumzo mahiri ikiwemo kujituma katika utafutaji.

Inadaiwa kuwa, jambo hilo lilimkasirisha Bi. Lushomo, ambaye alimtaka kuhama na kumpisha na kumwambia kuwa hana akili za kutosha kwani amekuwa akimlipa kodi ya kila mwezi kwa sababu nyumba wanayoishi ni yake.

Mara baada ya kuoneshwa hati, ya nyumba hiyo, inasemekana Martin alipoteza fahamu na kuzimia kitu ambacho kilisababisha Wananchi kumpa msaada wa kumwagia maji ili kumzindua kisha kumuwahisha Hospitalini.

Watafiti watakiwa kuwa msaada vivutio vya utalii
Wakulima mbogamboga kupatiwa maeneo ya wazi mijini