Kiungo Mshambuliaji kutoka Burkina Faso Stephen Aziz Ki amejiunga na Kikosi cha Young Africans, baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa michezo mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Aziz Ki alirejea nchini kwao baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Club Africain ya Tunisia, kwa ajili ya kupumzika na kupisha muda wa kutumia adhabu yake.

Afisa Habari wa Young Africans Ally Kamwe amesema Kiungo huyo amerejea kambini na kuanza maandalizi ya kujiwinda na mchezo wa kesho Jumamosi (Novemba 26) dhidi ya Mbeya City.

“Aziz Ki alianza mazoezi jana Alhamis (Novemba 24), alikua sehemu ya kikosi cha kwanza ambacho kitaikabili Mbeya City FC kesho Jumamosi Uwanja wa Mkapa, Wachezaji Wenzake wameonyesha kufurahia kurejea kwake, hii inatuonesha kuna upendo mkubwa katika kikosi chetu.” amesema Ally Kamwe

Kufuatia adhabu hiyo Aziz Ki alikosa michezo dhidi ya Kagera Sugar (Novemba 13), Singida Big Stars (Novemba 17) na mchezo dhidi ya Dodoma Jiji FC uliopigwa Jumanne (Novemba 22).

Simba SC kusajili watatu dirisha dogo
Simba SC yafanywa Shamba Darasa Kigamboini