Mtangazaji wa XXL ya Clouds FM, Hamisi ‘B12′ Mandi ameeleza kile anachoamini kinakosekana hivi sasa kwenye msitu wa wasanii wa Hip-Hop na Rap Tanzania, akilinganisha na ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.

B12 ambaye kwa mtazamo huru, hivi sasa anakidhi vigezo vya kuitwa mtangazaji mkongwe aliyeng’ang’ania nafasi ya kwanza ya mtangazaji bora wa vipindi vya redio vya burudani, amesema kuwa hivi sasa hakuna ushindani uliokuwepo hususan kwenye upande wa freestyle (mitindo huru).

Akizungumzia jinsi anavyokumbuka uwezo wa marehemu Godzilla kwenye freestyle, alisema yeye binafsi alikuwa shabiki wake mkubwa kwenye upande huo.
“Mimi mwenyewe nilikuwa shabiki mkubwa wa Godzilla, kama ambavyo mtu mwingine anavyosikiliza redio halafu anashangilia akimsikia na kusema ‘daah jaama anaweza,”B12 aliiambia Global TV.

“Pengo lao hawa jamaa, Ngwair na Godzilla haliwezi kuzibika. Halafu hata sasa hivi unaona hakuna ushindani wa freestyle kama wakati ule, Godzilla mshindani wake mkubwa alikuwa Nikki Mbishi,” aliongeza.

Marehemu Godzilla aliibuka na kung’aa kwenye muziki baada ya kushiriki shindano la mitindo huru iliyoitwa ‘Freestyle Battle’, yalianzishwa na DJ Fetty kama sehemu ya mradi wa XXL.

Mitindo huru ni sehemu ya nguzo na utamaduni wa hip hop ambapo msanii huonesha uwezo wa kughani bila kuandika, akitoa kichwani papo kwa papo.

Adaiwa kumuua mpenzi wake na kumtundika kwenye nyaya za umeme
Rais Buhari aamuru vyombo vya usalama kutokuwa na huruma na mtu