Washika bunduki wa Ashburton Grove, Arsenal wanaripotiwa kuhamisha mashambulizi ya usajili kwenye klabu bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG), huku wakimlenga mshambuliaji kutoka nchini Uruguay Edinson Cavani.

Arsenal wanahusishwa na mpango huo baada ya kuthibitishiwa hawawezi kumpata mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Real Madrid Karim Benzema ambaye alikua chaguo lao la kwanza katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

The Gunners waliamini hawataweza kumsajili Benzema, licha ya kuarifiwa mapema na uongozi wa klabu ya Real Madrid kwamba, dili hilo kutoweza kufanyika, lakini baadae mchezaji mwenyewe alianika msimamo wake hadharani kutaka kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambayo ilimsajili mwaka 2009 akitokea Olympic Lyon.

Cavani, mwenye umri wa miaka 28, anatajwa kuwa katika mipango ya meneja Arsene Wenger, kufuatia mambo kumuendea kombo kwenye safu ya ushambuliaji tangu walipoanza msimu huu, ambapo wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja, kufungwa mmoja na kuambulia sare mara moja.

Hata hivyo bado uongozi wa Arsenal haujathibitisha rasmi kama umehamisha nguvu za usajili kwa mshambuliaji huyo, licha ya kuelezwa wazi meneja Arsene Wenger atalazmika kufanya usajili kabla ya dirisha la usajili kufungwa Septemba mosi.

Cavani alisajiliwa na PSG mwaka 2013 kwa ada ya uhamisho wa paund million 55 akitokea Società Sportiva Calcio Napoli ya nchini Italia, na mpaka sasa ameshacheza michezo 79 na kuwafungia mabao 54 mabingwa hao wa nchini Ufaransa.

Jordin Spark Aifunza Billboard Kuandika Habari, Ni Baada Ya Kumtibua
Serikali Yakataa Ombi La UKAWA Kutumia Uwanja Wa Jangwani Jumamosi Hii