Chama cha ACT Wazalendo kinatarajia kuzindua kampeni zake za kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu hii leo Septemba 13, Visiwani Zanzibar.

Mkutano huo unatarajiwa kuzinduliwa na mgombea wa nafasi ya urais wa Serikali Mapinduzi ya Zanzibar kupitia chama hicho Maalim Seif Shariff baada ya juzi Septemba 11 Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC), kutupilia mbali pingamizi alizowekewa mgombea huyo wa urais katika kuwania nafasi hiyo.

Hii ni mara ya sita kwa Maalim Seif kugombea urais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, akitarajiwa kuchuana na wagombea 16 kutoka vyama vingine vya siasa.

Jana Septemba 12, Mgombea urais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia Chama cha mapinduzi (CCM), alizindua kampeni za Chama hicho Zanzibar.

Mwanamke aliyejikata mkono atupwa jela kwa utapeli
Mali: Jeshi kuunda serikali ya mpito