Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara amemtaka kocha wa Yanga kujifunza jinsi ya kuzungumza pindi timu yake inapofungwa.

Ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Istagram, ambapo Manara ameanza kwa kumsifia kocha wake, Patrick Aussems kwa kitendo cha kuwapongeza wapinzani wake Kagera Sugar kutokana na kiwango walichokionyesha dhidi yao, huku akimtaka kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kuiga mfano huo badala ya kulalamika kuwa wanaonewa.

Manara ameandika kuwa, “Tofauti ya kocha wa mpira na kocha wa Sunsumia au kibao kata!!. Unafungwa unawapongeza washindi na kukubali mapungufu yako, angekuwa yeye sasa!, “waamuzi wanatuonea, mimi nimefundisha Ulaya miaka arobaini”, ( ukigoogle ) huoni timu alizofundisha zaidi ya kufundisha kucheza ndombolo na mayenu ). “Ohh Simba inabebwa, leo sikushinda kisa Ajibu na Fei Toto na hawajala toka juzi!!,”

Aidha, baada ya kupoteza mchezo huo, sasa Simba inasalia na pointi zake 60 baada ya kucheza michezo 24, huku Kagera Sugar ikiwa katika nafasi ya 13 na pointi 39 baada ya kucheza mechi 33 mpaka sasa.

Hata hivyo, Simba inaendelea na ratiba ya kupunguza viporo vyake ambapo sasa inajiandaa kucheza na Alliance FC ya jijini Mwanza, April 23 katika dimba la CCM Kirumba.

Hakuna sikukuu kwenye kazi ya Umeme- Dkt. Kalemani
Wagombea ubunge waingia mitini na fomu, msimamizi awataja