Rais wa Panama ametangaza siku ya Jumatano kuwa siku kuu baada ya nchi hiyo kufuzu kwa mechi za kombe la dunia kwa mara ya kwanza kabisa.

Panama ilishinda Costa Rica mabao 2-1 mjini Panama City ikiwa ni mara ya kwanza tangu ianze kijaribu kupata nafasi hiyo mwaka 1978.

Kupitia ukursa wake wa Twitter rais Juan Carlos Varela‏ aliandika, “Sauti za watu zimesikika…Kesho ni siku kuu ya kitaifa.” Rais alisema kuwa wafanyakazi wa umma na wale wa makampuni ya kibinafsi watapumzika na pia shule hazitafunguliwa.

Watu nchini Panama walisherekea usiku kucha baada ya ushindi huo na wataishuhudia nchi yao ikishiriki katika michuano hiyo mwaka 2018 ambayo inaanza mwezi Juni mwaka ujao nchini Urusi.

Marekani ilikuwa katika kundi moja la kufuzu kwa nchi za kaskazini na kati mwa Marekani, lakini ikashindwa baada ya kupoteza kwa Trinidad and Tobago huku Mexico na Costa Rica wakifuzu.

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 12, 2017
Polisi Dar wasambaratisha mkutano wa Sheikh Ponda