Kombe la shirikisho nchini maarufu kama (ASFC), linaendelea katika hatua ya 16 bora ambapo jumla ya mechi 8 zitapigwa kuwania nafasi ya kucheza robo fainali.

Kati ya mechi hizo ipo ya vigogo Yanga dhidi ya Namungo FC ambayo itapigwa Jumapili hii huko mkoani Lindi. Wakati huo mabingwa watetezi Mtibwa Sugar wakiwa katika dimba la Azam Complex kukipiga na KMC leo saa 10:00 jioni.

Katika mechi nyingine Azam FC ambao wametoka kufungwa na Simba mabao 3-1 kwenye ligi kuu, wanakipiga na Rhyno Rangers ya Tabora siku ya Jumatatu kwenye uwanja wao wa Azam Complex.

Aidha, michezo hiyo yote inapigwa kwa mchezo mmoja tu ambapo mshindi inabidi apatikane huku mikwaju ya penalti ikitumika kuamua michezo ambayo matokeo yake ya dakika 90 yanamalizika kwa sare au sululu.

Hata hivyo, bingwa wa michuano hiyo anapata nafasi ya kuwakilisha nchi katika michuano ya kombe la shirikisho Barani Afrika pamoja na zawadi ya shilingi milioni hamsini.

Rais Omar al-Bashir wa Sudan atangaza hali ya dharula
Mpina apiga marufuku makongamano ya kumpongeza JPM