Siku mbili baada ya Marekani kutangaza kusitisha msaada wa zaidi ya shilingi trilioni moja za kitanzania kupitia Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) kutokana na kutoridhishwa na kufanyika kwa uchaguzi wa marudio na utekelezaji wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, Mashirika mengine yamejitosa kuziba pengo hilo.

Kiasi hicho cha fedha kilikuwa kimekusudiwa kutumika katika utekelezaji wa mpango wa kusambaza umeme vijijini na kupanua barabara za vijijini ikiwa ni awamu ya pili.

Akizungumza jana na vyombo vya habari, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango alisema kuwa Serikali haijashtushwa na uamuzi wa MCC kwani ilikuwa inatarajia matokeo hayo na ilijipanga tangu Disemba mwaka jana kutumia fedha za ndani na mashirika mengine.

“Haijatushangaza hata kidogo kwa sababu tulikuwa tumejiandaa kwa matokeo yoyote. Tutatekeleza miradi yetu kwa kutumia fedha za ndani na msaada kutoka kwa wadau wengine wa maendeleo,” alisema Dk. Mpango.

Akitaja mashirika ambayo tayari yameshatangaza kuzipa pengo la MCC, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, Felchesmi Mramba alisema kuwa tayari Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) wamekubali kugharamia miradi iliyokuwa inafadhiliwa na fedha za MCC.

Newcastle Utd Wapata Pigo Juu Ya Pigo
Magufuli apitisha Panga lingine huku