Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema kuwa Watanzania wapatao 9 wameuawa na wengine 6 kujeruhiwa nchini Msumbiji ambako walikwenda kujitafutia riziki.

Ameyasema hayo mkoani Mtwara eneo la mpaka wa Tanzania na Msumbiji ambapo amesema kuwa mauaji hayo yamefanyika Juni 26, 2019 ambapo pia watu wa Msumbuji kadhaa nao wameuawa.

”Waliofanya haya matukio tutawatafuta na nimeongea na IGP mwenzangu wa Msumbiji nimemuomba tukutane kesho Juni 30, 2019 ili tuongee juu ya tukio hili na mengine”, amesema IGP Sirro

Amesema kuwa amesikitishwa sana na vifo vya Watanzania hao ambao wamepigwa risasi na watatumia kila njia kuwapata waliofanya mauaji hayo.

Aidha, ametoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao pamoja na majeruhi 6 walionusurika kwenye mauaji hayo, ambapo amewataka wananchi watoe taarifa zinazoweza kusaidia kupatikana kwa wauaji hao.

Imeelezwa kuwa Watanzania hao huenda nchini Msumbiji wakati wa msimu wa kilimo kwaajili ya kulima na kujipatia mazao pamoja na kipato.

Video: Doto Biteko aonya, 'Wizi wa madini sasa ni zilipendwa'
LIVE DODOMA: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya TAKWIMU