Baadhi ya mambo mengi ambayo wadada wakiwa wanaenda kwenye usahili (interviews) wa kazi cha kwanza atazingatia muonekano.

Ndani ya jambo la muonekano ni mengi ambayo unaweza kuwa bado hujayajua kuwa ndio kikwazo cha kufeli katika usahili wako japo ulijibu kwa ufasaha katika maswali uliyo ulizwa.

Wazoefu na Wajuzi mbali mbali ambao wamekwishapitia katika mambo hayo wanatoa ushauri wa kuzingatia pindi unapokuwa umeitwa kwenye usahili. Hapa chini baadhi ya mambo ya kufanya au kuepuka wakati wa usahili. Kumbuka vazi kubwa kabisa ni ujasiri.

1. Wakati ukiwa unazingatia suala la muonekano hakikisha unaepuka mapambo yaliyo pita kiasi (make up) kwenye uso wako iki ni pamoja na urembo uliopitiliza,

make up

2. Chagua mtindo wa kitaaluma na weledi wa nywele zako . Mtindo wa nywele utakusaidi kuwa makini kusikiliza na siyo kuhangaika kuzitengeneza zikae vizuri wakati unajibu maswali.  kama nywele ni fupi ni vizuri ukazichana ili zionekane nadhifu.

hair

 

3. Tafuta kijifaili kizuri au pochi ajili ya kuweka  vyeti vyako au nyaraka mbali mbali (muhimu) kama zitahitajika wakati huo.

brif

4. Tafuta viatu  ambavyo unaweza kutembea navyo vizuri kwa kujiamini wengine hupendelea viatu virefu lakini ni vyema ukava vyenye soli fupi kutokana na mazingira kwa kuwa utakua mgeni katika maeneo hayo huwezi jua miundombinu ilivyo.

flat

5. Epuka nguo fupi sana inayokufanya usikae kwa amani ukabaki tu kuishikilia, Inategemea na aina ya kazi lakini ni vyema uka vaa  nguo ambayo itakuonesha upo nadhifu na siyo tena ikufanye uabike mble za watu.

short

Makinda atumbua wakurugenzi 9 NHIF, mabilioni yapigwa
Askofu Gadi Aandaa Mkutano Wa Kuiombea Tanzania