Makamu Mwenyekiti klabu ya Yanga, Frederick Mwakalebela, amesema wachezaji David Molinga ‘Falcao’ na Mustafa Suleiman hawatatumika katika mchezo dhidi ya Pyramids katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam, Mwakalebela amesema wachezaji hao hawataweza kutumika sababu ya kukosa vibali kutoka shirikisho la soka barani Afrika (CAF).

Mwakalebela ameongezea kuwa wataweza kutumika endapo timu itangia katika hatua ya makundi na katika michezo ya Ligi Kuu Bara wataendelea na kazi kama kawaida.

Tangu michuano ya kimataifa ianze, wachezaji hao hawajashiriki mashindano hayo sababu ya kukosa vibali.

Yanga itakuwa na kibarua cha raundi ya kwanza dhidi ya Pyramids kutoka Misri Oktoba 27, mechi itayaochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Krasimir Balakov abwaga manyanga
Watanzania 19,681,259 wajiandikisha uchaguzi, Dar yaibuka kinara