Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 43, anashikiliwa na polisi nchini Kenya kwa tuhuma za kumuua kijana mwenye umri wa miaka 24 aliyemkuta na binti yake mwenye umri wa miaka 16, anayesoma shule ya msingi.

Inaelezwa kuwa Juzi, John Odhiambo Juma, alimpiga hadi kumuua Benson Onyango baada ya kuingia ndani ya nyumba yake na kumkuta na binti yake huyo ambaye hakuonekana nyumbani kwa siku nzima, katika Kaunti ya Siaya.

“Mtuhumiwa alipata taarifa kuwa binti yake yuko ndani ya nyumba ya Onyango. Alipofika aliwakuta wawili hao ndani, ndipo kwa hasira alianza kumpiga Onyango kwa lengo la kumuadhibu. Lakini kwa bahati mbaya alianguka sakafuni na kupoteza maisha,” alisema Ambrose Ogema, Mkuu wa eneo la Mageta.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alijaribu kuondoka katika eneo hilo, lakini alikamatwa na wananchi waliokuwepo na kukabidhiwa kwa jeshi la polisi.

Mesut Ozil hatarini kupoteza nafasi Arsenal
Luis Suarez kusubiri hadi Disemba

Comments

comments