Mwanaume mmoja nchini Uganda, Isma Ssesanga anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kike ambaye alimtuhumu kwa kula chakula walichokuwa wamechua kwenye sherehe moja waliyohudhuria.

Ilikuwa siku ya jumapili, Isma na wanawe watatu walienda kwenye sherehe ambapo walikula na kusaza, kisha wakabeba chakula kilichobaki na kurudi nacho nyumbani.

Ilipofika majira ya jioni baba yao alienda kuangalia mpira, mechi ya ligi kuu Ueingereza, ndipo watoto wakatumia mwanya huo kula chakula hicho hivyo baba yao aliporejea akakuta chakula kimeliwa chote.

Mtoto Salama Nassanga mwenye umri wa miaka 10 alifariki dunia jana, baada ya kupigwa vibaya na baba yake.

Imeelezwa kuwa mwanaume huyo alianza kwa kuwapiga watoto wake wawili wa kiume kabla ya kuanza kumpiga mtoto wake wa kike ambaye ndiye mkubwa, wote akiwatuhumu kwa kula chakula hicho.

Kwa mujibu wa mashuhuda ambao ni majirani wamesema mtoto Salma alifariki wakati baba yake akiendelea kumpiga huku mwanaume huyo akisema alifariki alipojaribu kukimbia na kujigonga kwenye kitu kigumu.

Mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa hospitali ya Kayunga kwaajili ya uchunguzi zaidi.

Tetesi za soka: Solskjaer akataliwa Manchester, Pulisic afikiriwa Chelsea
Tim Howard atundika Gloves