Baba mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba ambaye ni mlemavu wa mguu anayeishi mkoani Shinyanga  amempigia simu Waziri wa habari sanaa, michezo na utamaduni, Harrison Mwakyembe akimtaka amkumbuke katika mikataba ya mwanaye aliyowahi kusaini na makampuni mbalimbali enzi za uhai wake.

Baba Kanumba amesema hayo akidai kuwa yeye ndio aliyemlea Steven Kanumba mpaka alipokuwa mkubwa hivyo anaomba akumbukwe ili aweze kupata haki yake kupitia mikataba.

”Namuomba sana Mwakyembe anikumbuke na mimi kwenye kusaini fedha za mikataba ya mwanangu iwapo zitatoka kwani nami nina haki maana nilimlea sana akiwa mdogo mpaka akawa mkubwa nikamuuliza anachagua kukaa wapi ndipo akachagua kwenda kuishi kwa mjomba wake. “Kwa sasa mimi nimekuwa mlemavu wa miguu hivyo naomba na mimi nikumbukwe, na mimi nina haki msinisahau,” alisema baba Kanumba.

Aliendelea kusema kwamba anaiomba serikali iingilie kati suala hilo na endapo fedha hizo za mikataba ya Kanumba zitatoka basi wasaini wote yeye na mama Kanumba na siyo waangalie upande mmoja yaani mama tu.

Baba Kanumba ameibuka na suala hilo mara baada ya waziri Mwakyembe kutangaza kuanza kusimamia rasmi mikataba ya wasanii waliodhurumiwa na makampuni mbalimbali waliofanya nao biashara na kwa kuanzia Mwakyembe aliahidi kuanza kukagua mikataba ya Kanumba na Mzee Majuto aliyeibua suala hilo mara baada ya kukosa hela ya kufanyiwa matibabu nchini India kufuatia upasuaji aliofanyiwa hapo awali.

 

Loris Karius apata kimbilio
Argentina yaibamiza Haiti, Messi atamba

Comments

comments