Binti Oyinye Aguluka ameuawa kwa kukatwa na panga na baba yake mzazi, Cletus Aguluka, masaa machache kabla ya harusi yake.

Binti huyo ambaye anaishi nchini Nigeria yalimkuta masahibu hayo akiwa amelala usingizini, baada ya baba yake aliyekuwa amelewa kuja na panga na kumshambulia.

Aidha, Mama Mzazi wa marehemu aliyetambulika kwa jina la  Georgina  amesema kuwa mume wake alirudi usiku akiwa amelewa na kuwauliza watoto wake mahali ilipo tochi yake.

Baba huyo alikuja na panga na kuanza kumshambulia binti yake huyo ambaye alitakiwa kufunga ndoa Jumamosi ya Juni 2, 2018.

Hata hivyo, Mtuhumiwa huyo alikamatwa na wazee wa kijiji na kupelekwa kituo cha polisi, ambako anashikiliwa mpaka sasa.

Museveni ashinikiza Kanisa kumtangaza Nyerere Mtakatifu
Safari ya Maria na Consolata imetuachia funzo kubwa sana