Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa baba wa mtoto mwenye asili ya China aliyesambazwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya mama yake kufika ofisini kwake akidai ametelekezwa anatafutwa.

Ameyasema hayo hii leo alipokuwa akifanya mahojiano maalum na TBC, ambapo amesema kuwa tayari wamesha wasiliana na ubalozi wa China na kutuma nyaraka zote ili aweze kutafutwa mara moja.

“Kuhusu yule mtoto mwenye asili ya Kichina, tumesha wasiliana na wenzetu wa ubalozi wa China, na tumewatumia nyaraka zote ili aweze kutafutwa,”amesema Makonda

Hata hivyo, Makonda amesema kuwa kama baba wa mtoto huyo hatapatikana basi serikali itakuwa na jukumu la kumlea mtoto huyo.

 

 

Fatma Karume amrithi Tundu Lissu TLS
Mtoto wa Mandela awacharukia wanafiki wa Mama yake

Comments

comments