Baba wa Rihanna Ronald Fenty ameeleza kuwa alishamsamehe Chris Brown aliyemdunda mwanae Rihanna mwaka 2009 na kumpigia chapuo katika mwezi huu unaoitwa ‘mwezi wa mapenzi’.

Mzee Fenty ameonesha kusikishwa na kitendo cha Rihanna kuimba tena kuhusu tukio hilola kushambuliwa na Chris Brown aliyekuwa mpenzi wake, katika wimbo wa Love in The Brain unaopatikana kwenye albam yake mpya ‘Anti’.

“It beats me black and blue but it f**** me so good / And I can’t get enough,” RiRi anasikika kwenye sehemu ya wimbo huo.

Akiongea na Mirror, Fenty amesema kuwa anamkaribisha Chris kwenye familia yake kwa kuwa anampenda na angependa wawili hao wawe pamoja tena kama zamani.

“Ninapenda simulizi lake lakini huu wimbo ulikuwa mgumu kuusikiliza. Chris ataendelea kuwa na nafasi katika familia yetu siku zote na ndani ya moyo wangu. Ananiheshimu, ananiita ‘baba’ na nampenda- mbali na kilichotokea. Ana kipaji na yuko ‘humble’. Naunga mkono wakwe pamoja,” alisema.

Mwaka 2009, Chris Brown alimpiga na kumpa majeraha makubwa Rihanna aliyekuwa mpenzi wake na kufikishwa mahakamani ambapo sheria ilimkata vilivyo. Hata hivyo, wawili hao walirudiana baadae na kutosana tena.

Penzi la Nicki Minaj lamponza Meek Mill, Jaji amshushia nyundo ya kifungo
Hotuba ya Rais Magufuli yazua 'Zogo', Wadai kaiteka mahakama kwa ahadi ya fedha