Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amefanya pangua pangua katika kikosi chake kwa kuwang’oa baadhi ya vigogo katika kikosi cha kwanza ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuunda jeshi la ushindi.

Baada ya kukaa na kikosi hicho kwa vipindi viwili vifupi msimu wa 2013/14 na 2014/15, Pluijm amebaini kuwa na wachezaji wasiostahili kucheza namba wanazozitumikia kutokana na aina ya uchezaji wao inayokinzana na mifumo na falsafa zake.

Miongoni mwa wachezaji vigogo wa Yanga wanaoonekana kuelekea kupoteza nafasi katika kikosi cha kwanza, ni beki wa kushoto wa muda mrefu, Oscar Joshua. Nafasi ya Oscar inatishiwa kuchukuliwa na Haji Mwinyi, kijana ambaye anayeweza kukidhi matakwa ya Mholanzi huyo.

Pluijm anonekana kumkubali zaidi kijana huyo baada ya kumshuhudia mapema mwaka huu kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar akiwa na kikosi cha KMKM.

Mwinyi ameendelea kutishia kuchukua nafasi ya Joshua baada ya kuonesha kiwango kizuri zaidi katika mechi mbili za kirafiki alizocheza kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame.

Klabu Ya Ulaya Yawaumbua Simba Kuhusu Emmanuel Okwi
Mkanda Wa Ngono Wa Mama Mtoto Wa Rick Ross Wamfilisi 50 Cent